Sospeter, Dar es Salaam
Kwa sasa hivi, hali ilivyo, tunaona bado kuna nyuso za viongozi ambao wanaonekana ni watu wazima zaidi. Hii hali mimi nafikiri ingebadilika kidogo. Wapo watu ambao wanamaliza vyuo mpaka leo hii wanahitaji kufanya kazi. Kwa hiyo ni vyema wale ambao umri wa kufikia kustaafu wamefikia, basi wastaafu. Ili wapishe wale ambao wanahitaji kufanya kazi, waendelee kufanya kazi, nao wajifunze uongozi unavyokwenda.
Right now, the way it is, we see many leaders who are very old. I think it would be good if this situation could change a little. There are people who have finished University and need jobs. Therefore it is better if the ones who have reached retirement age just retire. So that they make space for the ones who need a job, so that these can go ahead and work and learn about leadership.
