Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

Ajira

elimu

Jina

jahrean Iringa

Maoni

mimi nilikuwa naomba selikali iboreshe nyumba za walimu na mazingira ya usafili kwani walimu wana mazingira mabaya ya kimaisha mishahara wanachelewa kuipata hasa malipo ya uzeeni na mishahara wawapo kazini ili walimu wawe na moyo wa kuwafundisha watoto. Hii itapunguza watoto na walimu kukimbilia tuisheni na shule binafsi

Simu

Barua pepe

jahrean@yahoo.com
Vote Result
----------

ajira

Jina

Suzana Ruhasha

Maoni

Ninashangazwa ninapoona tangazo la kazi lakini wanataka uzoefu si chini ya miaka mitatu,je mtu aliyemaliza chuo afanye kazi wapi?

Simu

Barua pepe

ruhashasuz@yahoo.com
Vote Result
----------

WATAALAMU WAPEWE KAZI KULINGANA NA ELIMU NA FANI ZAO.

Jina

JOSEPHAT KAHENDAGUZA

Maoni

NAPENDA KUTOA MAONI YANGU KUHUSU WATAALAMU WETU KUPEWA KAZI TOFAUTI AU CHINI YA NGAZI YA UWEZO WAKE KITAALUMA KUNARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA NCHINI NA KUMFANYA MTU KUDHALALIKA NA KUKOSA THAMANI YA ELIMU YAKE. KITU AMBACHO KINAMFANYA AFIKIRIE AIDHA KUHAMIA MAHALA PENGINE AU NCHI NYINGINE AMBAPO WANATAMBUA UMUHIMU WA MTAALAMU KAMA HUYO. MFANO, MTU AMBAYE NI MHANDISI MKUU WA MASWALA YA MAJI NA MAZINGIRA, MWENYE SIFA ZA SHAHADA MBILI ZA JUU( BSC NA MASTERS DEGREES)PAMOJA NA UZOEFU WA MIAKA ZAIDI YA KUMI KATIKA NCHI ZA ULAYA NA AFRICA ANAAMBIWA AENDE WILAYA CHINI YA TECHNICIAN IV AMPANGIE KAZI ZA KUFANYA. KITU AMBACHO MTU KAMA HUYU HATA KAMA ANA MPANGO MWENDELEVU HATAWEZA KUFANYA KAZI NA UWEZO WA KUELEWANA KITAALUMA HAUPO. HIVYO UTENDAJI KAZI HAUTAZAA MATUNDA YOYOTE.

Simu

0786142051

Barua pepe

jkahendaguza@yahoo.co.uk
Vote Result
----------

AJIRA

Jina

CHIKAKA

Maoni

Waajiri wengi wa sekta binafsi ni wanyonyaji (wa muda wa waajiriwa),wengi uwashawishi wafanyakazi( hasa wahitimu ambao hawajawahi kuajiriwa, pengine hawazitambui vizuri haki zao )kwa ahadi nyingi ambazo uwa ni za uongo, na kuwasainisha mikataba yenye kukandamiza haki za mfanyakazi.

Simu

Barua pepe

jmfalme@yahoo.com
Vote Result
----------

waajiri wasiwazuie wafanyakazi wao kujiendeleza kielimu

|

Jina

Pwani Mwankanda, wa Kiwira, Tukuyu.

Maoni

Tupo kwenye dunia ya utandawazi,sayansi na tekinolojia. Dunia inayo hitaji watu wenye elimu ya kutosha. Lakini, kitu cha kusikitisha ni kwamba, kuna baadhi ya taasisi za serikali na za binafsi hapa tanzania zinawazuia wafanyakazi wake wasijiendeleze kielimu. Viongozi wa taasisi hizi wamekuwa wakiweka vikwazo vingi kwa mtu anaye taka kujiendeleza kielimu. Hii yote inasababishwa na viongozi hawa kuwa na woga wa kupoteza madaraka kwa vijana wenye nia, ari na uwezo wa kujiendeleza kimasomo. Mimi naona serikali itafute maoni toka kwa wafanyakazi,ili kubaini viongozi wenye tabia ya kuzuia wafanyakazi wao wasijiendeleze kielimu. mara watakapo bainika viongozi hawa wafukuzwe kazi, kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu.

Simu

0741663701

Barua pepe

Vote Result
----------

Kevin, Dar es Salaam

Kevin

Namuomba Rais alioko madarakani kwa sasa atazame ajira zetu. Sisi tulio katika mabaa, katika ngazi za wale tunaofanya kazi ndani, aweze kutazama ajira zetu tuweze kupewa ajira kwa baada ya miezi sita. Maana hizi zimekuwa ni kero kwetu hatupewi ajira mpaka baada ya miaka mitatu tunafukuzwa bila ya kuwa na ajira ya aina yoyote.


I ask the current president to consider our employment conditions. We who work in bars as well as those who work in households, he should look into our employments so that we can get permanent employment after a period of six months.

Vote Result
----------

Emanuel, Bagamoyo

|
Emanuel

Wengi wananchi wana talent kubwa sana ya kuweza kufanya vitu ambavyo watu wengine hawataweza kufanya. Lakini kutokana na umaskini wa nchi yetu vijana wengi wanakuwa wanashindwa kupata ajira au wengine wanashindwa kuendeleza talent zao. Naona, kama Bagamoyo tukijengewa studio hapa itaweza kunisaidia mimi na watu wengine ambao watakuwa na talent za muziki.


Many citizens are very talented and can do things that others can't. But because this is a poor country many young people don't manage to get a job and can't develop their talents. I believe, if we could get a studio to be built in Bagamoyo, it would help me and other people who have a talent for music.

 

Vote Result
----------

Jaqueline, Simanjiro

|
Jaqueline
Ajira kwa watoto walio chini ya umri, imekithiri sana humu nchini. Wengi wao huishia kudhulumiwa, wananyanyaswa na hata kufukuzwa. Kinachotokea hapa ni kujiingiza katika madawa ya kulevya, udokozi na ukahaba. Na matokeo ya ukahaba ni kupata mimba za utotoni. Hivyo basi, tunaomba mabalozi wa nyumba kumi wapewe jukumu la kuangalia kila nyumba yenye msichana wa ndani.

Child labour has become too common in this country. Many of them are denied their rights, they get harrassad and are chased away. Then what happens is that they start with drugs, theft and prostitution. And the outcome of prostitution is child pregnancy. Therefore, we ask the ten cell leaders to take responsibility for keeping an eye on each household that employs a housegirl.

Vote Result
----------

Sulemida, Lushoto

|
Sulemida, Lushoto (p)
Ningependa kuwa mwanasheria... nimependa kazi hii kwa sababu ni wachache ambao wanatendewa haki. Ukichukulia wasichana, mtu anaenda kuomba kazi sehemu anaambiwa kama sio jinsi yake, aliyemkuta anamwambia "nifanyie mapenzi ili nikupe kazii" Hawa, mimi ningekuwa mwanasheria, ningeona ni haki ya msichana apewe kazi endapo ana elimu inayohusiana na kazi hiyo.


I'd like to be a lawyer... I like this profession because here, few people are treated with justice. Take girls for example, a girl asks for a job some place but is told that it's not the way it is, the employer tells her "make love with me first if you want the job". If I was a lawyer, I would see to that this girl has a right to that job as long as she is qualified for it.

Vote Result
+++++++++-

Syndicate content