Siasa
Uongozi na Katiba
Submitted by Mwananchi on Fri, 2007-02-16 09:58. SiasaJina
MpigaKura
Maoni
1. Viongozi katika ngazi zote za utawala wawe wa kuchaguliwa ili kuendana na mfumo wa vyama vyingi. Si sahihi kuwa na halamashauri iliyo chini ya chama A halafu kukawa na mkuu wa wilaya akisimamia maslahi ya chama B.
2. Majukumu ya Waziri mkuu yaonganishwe na yale ya makamu wa raisi. Mmoja kati ya wawili hawa anapaswa kuondoka.
3. Katiba isukwe upya na ishirikishe wananchi na si ya kujifungia.
4. Mwanachi asiwe na nguvu wakati wa uchaguzi tu, kama kiongozi anafanya vibaya awajibishwe hata kabla ya miaka mitano.
Simu
UONGOZI
Submitted by Mwananchi on Sat, 2006-10-14 10:58. SiasaJina
Valo Niame
Maoni
Viongozi wa awamu ya nne wamegubikwa na ziara na seminar zisizo na faida. wanatumia gharama kubwa katika semina na ziara, hela ambayo ingetumika katika maendeleo, mfano mahospitali na mashuleni.
Simu
0786387503
WOTE TUNA HAKI
Submitted by Mwananchi on Fri, 2006-10-13 07:45. SiasaJina
Maston W. Mwakila
Maoni
Mimi huwa nashangaa sana kuona viongozi wanaingia mikataba mikubwa mikubwa na mashirika ya nje ya ukopeshaji lakini wananchi mkitaka kuiona wanang`aka. Mbona kulipa sisi wananchi wa kawaida ndio walipaji wakubwa? Mnadhani kupewa mamlaka ya kusaini mikataba kwa niaba yetu ndio mna akila sana,ni mgawanyo wa madaraka tu. Kama hakuna mizengwe na rushwa katika mikataba hiyo na kama kweli mlifanya kwa nia njema ya maendeleo ya nchi yetu mbona mnaogoba kutuonyesha? Tunawasiwasi na mashaka katika maamuzi yenu. Kama mko safi weka mambo hadharani!
Simu
Mawaziri kujiuzia nyumba
Submitted by Mwananchi on Fri, 2006-09-15 17:05. SiasaJina
John
Maoni
Kitendo cha mawaziri kujiuzia nyumba za serikli sio cha kiungwana kwani mawaziri sio wafanyakazi wa serikali, ikiwa chama kikimfukuza uanachama na uawaziri hata kuwa nao, je nyumba atairudisha?
