Elimu
Serikali ikubali kukoselewa na kutafanyia utafiti matangazo yatolewayo!
Submitted by Mwananchi on Wed, 2007-02-07 20:53. ElimuJina
Mwanaharakat wa maendeleo ya maendeleo ya nchi.
Maoni
Maoni yangu ni kuwa imefikia wakati sasa Serikali ikubali kukoselewa pale ambapo ukweli huko wazi juu ya dosari za utekelezaji wake wa masuala ya elimu.
Hatua ya kukurupuka tu na kufungia vyombo vya binafsi au Taasisi zinazoikosoa kwa kupitia matangazo yake kwa vyombo vya habari kama Redio ,Television na vipeperushi mbalimbali,Lengo si kukosoa kuwa serikali haiwajibiki ipasavyo,la asha!!! lengo ni kuwakumbusha kuwa yapo maeneo mengine mipango iliyopo inakwenda kinyume na mkakati madhubuti wa kuyainua maisha ya kila mtanzania kwa kumpatia elimu inayostahili na iliyo bora na kumwezesha kujikwamua na hali halisi ya maisha na kuondoa utegemezi kwa asilimia kubwa.
Pamoja hilo nashauri kuwepo na nia na hatua madhubuti za Serikali kufanya uchambuzi wa kina wa matangazo hayo na kuchukua hatua za kuyarekebisha.
Pia nashauri Taasisi na Vyombo vingine vilivyo nje ya serikali kutokata tamaa katika kufichua yale ambayo kwa njia mmoja au nyingine yanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Nchi hii ni yetu sote na unapoamua kuamasisha maendeleo ya nchi kwa wananchi na ukasikilizwa basi ni vyema pia ukawa tayari kukubali kukosolewa!
Asanteni,
Mwanaharakati wa mageuzi ya maendeleo ya nchi.
Simu
0784844940
UCHANGIAJI WA ELIMU YA JUU KWA 40%
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-09 10:41. ElimuJina
Jonas J.Kimati
Maoni
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha kilimo Sokoine.Kinachoniuma ni kuona wanafunzi wanateseka kuhusu suala zima la mikopo hasa kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu.Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanalipiwa 60% ya garama zote ikiwa ni ada,malazi,chakula na mengineo.Je,hizo 40% watapata wapi huku angali ni watoto wa wakulima wenye kipato duni?Mfano,ada wanayotakiwa kuongeza ni wastani wa laki tano.Si hayo tu,tumejionea wenyewe ni jinsi gani wanafunzi wa mwaka wa kwanza wananyimwa malazi baada ya kufunguliwa chuo tarehe 08/01/2007 wakitakiwa kukamilisha ada kwanza.
Ninachoweza kusema mimi,kulikuwa na utaratibu mbovu wa taarifa kuhusu ushirikishwaji uchangiaji wa gharama za elimu ya juu kwa 40%.Wazazi wengi hawafahamu kuhusu hilo na watakaomia ni wanafunzi.Inabidi bodi isahau kuhusu uchangiaji wa elimu na itoe mkopo kwa 100%,mwaka ujao wa masomo iandae programu nzuri na kila atakayechukua fomu za kujiunga na chuo chochote ajue atachangia kwa asilimia fulani.
Simu
0713803083
Salome, Iringa
ElimuShule za msingi ada zimefutwa, lakini michango imezidi kupita kiasi. Inapofungwa shule kila kichwa cha mwanafunzi ni shilingi elfu sita, michango kila mwezi ni shilingi mia mbili, ambapo yaani hiyo ni kero kwetu sisi wazazi ambapo yaani ni bora ingerudi ada kuliko ile michango ya siku zote.
Primary school fees have been abolished, but the contributions we are supposed to pay are just too much! When the school closes we pay Tsh.6000 per pupil, we pay a monthly contribution of Tsh.200 and this really annoys us as parents. We would actually prefer to pay fees rather than contributions every day.
Bittony, Mbeya
Elimu
Suala zima la kucheleweshwa kwa malipo, ambao Mwanafunzi anatakiwa alipiwe haraka zaidi ili aweze kusoma kwa kutulia. Leo limekuwa ni tatizo kubwa, nafikiri linamgusa kila mwanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya juu, na bodi yetu kwa kweli nafikiri iliharakishwa kupewa majukumu makubwa ikiwa bado haijajiandaa kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote kwa wakati mmoja.
The whole issue of delayed payment of fees that should normally be paid to allow a student to concentrate on his studies: there is currently a big crisis and I think it affects every student of higher learning institutions. I really think our board was given a big task, way before it was ready to handle and address the needs of all students at once.
KUBORESHA ELIMU
Submitted by Mwananchi on Tue, 2006-11-07 15:22. ElimuJina
PATRICK NKANDI NANGALE
Maoni
Mimi ni mmoja wa wanaharakati wa elimu,napenda kuishauri serikali hasa katika suala zima la matatizo yanayowakumba wanafunzi wa sekondari na shule za msingi,naiomba serikali ianzishe Association za wanafunzi ambazo zitafanya kazi katika ngazi ya wilaya,mkoa na taifa na katika ngazi ya mkoa na wilaya zisimamiwa na afisa elimu kama mlezi mkuu ili kuwawezesha wanafunzi kukutana na kujadili masuala yao mbalimbali.Na katika ngazi ya Taifa katibu mkuu wa wizara ya Elimu ndiye anatakiwa kuwa mlezi wa association. Ambazo zinawezwa kuitwa BUNGE LA WANAFUNZI.
Simu
0753571616
Aibu kwa Taifa
Submitted by Mwananchi on Mon, 2006-10-30 13:49. ElimuJina
Ayasi Ramadhani
Maoni
Kuhusu elimu,Naomba hata wizara elimu waweke kingereza shule ya msingi maana tuna aibika tunapo fika nchi za kigeni maana kuongea unashindwa unabaki unajing'ata hii yote inatokana na Foundation mbovu mtu anaenda kujifunza kingereza baada ya kumaliza kidato cha nne,Naomba wizara ya elimu wajaribu kuliangalia hili swara vizuri,Maana hata wa Tanzania wanshindwa kufanya biashara nchi za nje au na wageni,Nafahamu kwamba tuna upeo na biashara lakini bila lugha za kimataifa hutafika mbali tutaishia Tanzania
Simu
elimu
Submitted by Mwananchi on Fri, 2006-10-20 15:23. ElimuJina
Farid Saleh
Maoni
ok .ningependa kuchangia ktk suala zima la elimu kwa upande wa zanzibar kwa kweli wanafunzi hawatendewi haki hasa ktk mashule ya serikali .kwa hiyo naomba kiwepo kitengo maalum ambacho kitashugulikia suala la elimu kwa visiwani na hata bara .Kitengo hiki kiwe ni kama kimbilio kwa wanafunzi pindi haki inapokosekana
Simu
0777873704
maoni
Submitted by Mwananchi on Thu, 2006-10-12 15:41. ElimuJina
amoni chrizostom
Maoni
maoni yangu ni kwamba monitor/kiranja aheshimiwe darasani nayeye akieshimiwa asijione mali kuwa yeye ni mtu katika jamii kwa kuwanyanyasa wenzake.
Simu
Mikopo kwa Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu
Submitted by Mwananchi on Mon, 2006-09-25 15:31. ElimuJina
Respicius Didace
Maoni
Suala la mikopo kwa wanafunzi wa taasisi za Elimu ya Juu sasa hivi ni tatizo ambalo limetawala vyombo vya habari. Ni maoni yangu kuwa kabla ya kusema kuwa wanaofaa kupata mkopo ni wale wanafunzi wenye DIVISION ONE (Wanaume) au DIVISION ONE na DIVISION TWO (Wanawake)ni lazima tufuatilie huko vyuoni kuona kama hayo matokeo ya kidato cha sita yana uhalisia katika matokeo ya vyuoni. Hapa namaanisha kama ni kweli waliopata DIVISION ONE huendelea kuongoza )vyuoni. Mimi naamini kuwa kuna wanafunzi wanapata madaraja ya chini kulingana na aina ya shule wanazosomea au kwa sababu nyingine mbalimbali, hawa wanapokuja vyuoni pengine na DIVISION TWO au THREE zao hufanya vizuri sana hata kuliko wale wa DIVISION ONE. Kutoa mikopo kwa madaraja kutawakosesha watoto wa walalahoi haki yao yamsingi ya elimu. Nadhani pia, ni kuwahukumu bila kuwasikiliza. Naamini siku moja tutakuja kuulizwa tulisema nini kuhusu haya. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Simu
swali
Submitted by Mwananchi on Thu, 2006-09-21 11:07. ElimuJina
gift
Maoni
kwa nini? wanafunzi wa chuo kikuu hawathaminiwi kuhusu mkopo?
