Mazingira
Utunzaji wa mazingira
Submitted by Mwananchi on Thu, 2007-02-15 18:45. MazingiraJina
Mrs T. E. Mshana
Maoni
Ni vema sana kama tutajali mazingira yanayotuzunguka sisi wenyewe na mahali pengine popote.
Inashangaza kumuona binadamu mwenye akili timamu, anapotupa taka taka mahali pasipo na eneo la kuhifadhia taka-taka.
vitu kama karatasi, maganda ya pipi, n.k.
hebu tuwe wastaarabu jamani. Nawaomba sana wamiliki wa magari binafsi na ya abiria wajitahidi kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka kwenye magari yao, waige mfano wa dala dala za Mwenge- Kariakoo.
Simu
USALAMA WA ABIRIA UBUNGO BUS TERMINAL
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-16 11:49. MazingiraJina
Kasele Kwikima
Maoni
Licha ya jiji kutoza sh. 200 Kwa kila abiria na wasindikizaji kwa ajili ya huduma zote ndani ya kituo hicho lakini wameshindwa kuwajali wadau wao hao kwani hakuna mahali salama kwa mvua na jua kwani mara ukatapo tikiti unatembea umbali mrefu juani, katika mvua au tope bila kizuizi chochote. Sehemu pekee yenye paa ni sehemu ya kushushia abiria umbali wa kilomita 0.8 toka magari yaendayo dodoma, morogoro, tanga, iringa, mbeya na sehemu kadhaa. Abiria waendao arusha moshi tu ndio wanaweza kunufaika na eneo hilo. Tatizo lingine ni utozaji ada wakati wa kutoka. Nilimsindikiza mtu kwa kutumia usafiri wa taxi. Kisha taxi ile kuondoka. Nilisubiri kwa muda wa nusu saa basi la iringa liondoke nihakikishe msafiri ameondoka. Mfukoni nilibaki na sh. 400 Tu nauli ya kunirudisha nyumbani mbagala charambe. Nilipofika getini nikadaiwa sh. 200 Ili nitoke. Sikuwa nayo kwani nauli ya mbagala kwa sasa ni sh. 300. Ilibidi mtoza ada anipitishe kwa sh. 100 Bita kunikatia tikiti anisaidie. Ilikuwa ni rushwa na nathubutu kutamka nilitoa rushwa ili nitoke.
Simu
0773 833383
Ibrahim, Mbeya
MazingiraMazingira ya hapa stend, tunashukuru sana wametutengenezea stend nini lakini kuna mambo yanatukera kama tuna hiyo chemba hapo. Hiyo chemba huwa inafika muda mvua imenyesha unakuta chemba inacheuwa harufu harufu, vijana wanashindwa kukaa hapo. kwamfano achana na hiyo chemba mitaro hii, hii mitaro yenyewe huaga inaziba maji yanaanza kutokea kwenye vishimo.
The state of the bus station: we are grateful that it was repaired, but we are concerned about the sewage system, like this tank here: sometimes when it rains it bursts and stinks so badly, that the young people can't stay around here. Another example is the drainage system that blocks so that the water leaks out of small holes.
Newton, Mbeya
MazingiraTunakatazwa kwamba tusikate miti na kuchoma mkaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, hapo hapo bili ya umeme inakuwa kubwa, saves line nayo inakuwa kubwa. Tungeliomba kwamba bei ya umeme ishuke chini ipunguwe yaani kiwango cha uingizaji umeme ndani saves line iwe chini kisha matumizi nayo yawe chini hapo ndio unaweza ukadhibiti suala la ukataji miti.
We are prohibited from cutting trees and burning charcoal for home use, but at the same time the electricity bills and the service charges are enormously high. We would like the electricity prices to be reduced and the installation
Mazingira
Submitted by Mwananchi on Fri, 2006-11-03 10:03. MazingiraJina
Godlove Mtengela
Maoni
Maoni yangu ni kuhusu Mazingira, mimi kwa mtazamo wangu suala la mazingira linaniumiza sana, Maana nyumba hizi tunazoishi ni chafu sana ndio maana hata magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu haviwezi kwisha kama suala hili halitatiliwa mkazo maalum. Sioni sababu kwamba kweli Serikali imeshindwa kabisa kudhibiti suala hili la uchafu kila sehemu, kuna haja gani kuwa na Balozi, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, Diwani, Mbunge nk..., Balozi anashindwa nini kupitia zile nyumba zake kumi na kuhakikisha zinakuwa safi? Inawezekana kabisa kwamba hawezi kufuatilia kwa sababu nyumba zao ndio zinazoongoza kwa uchafu. Huwa napata shida sana kuona uchafu umezagaa kila sehemu, Watanzania tumeshindwa tumeshindwa kweli kudhibiti suala la uchafuzi wa mazingira? utakuta baadhi ya nyumba mitaani maji machafu yanatiririshwa barabarani. Ni kero kweli kwangu binafsi.
Simu
Usafi katika manispaa ya Zanzibar
Submitted by Mwananchi on Thu, 2006-09-28 07:11. MazingiraJina
Fatma
Maoni
Suala la usafi katika manispaa ya Zanzibar. Utakuta askari wa jiji wanakimbizana na wafanyabiashara wa samaki na huku katika manispaa hiyo hiyo kuna mifugo tele inayozurura bila uangalizi wa mtu yeyote. Maoni yangu ni kuwa hao wafanyabiashara wangepewa masharti ya kuhakikisha eneo wanalofanyia kazi ni safi kila wakati na hao askari wa jiji wakashughulikia tatizo la mbuzi waliotapakaa katika manispaa hiyo
