UCHANGIAJI WA ELIMU YA JUU KWA 40%
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-09 10:41. ElimuJina
Jonas J.Kimati
Maoni
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha kilimo Sokoine.Kinachoniuma ni kuona wanafunzi wanateseka kuhusu suala zima la mikopo hasa kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu.Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanalipiwa 60% ya garama zote ikiwa ni ada,malazi,chakula na mengineo.Je,hizo 40% watapata wapi huku angali ni watoto wa wakulima wenye kipato duni?Mfano,ada wanayotakiwa kuongeza ni wastani wa laki tano.Si hayo tu,tumejionea wenyewe ni jinsi gani wanafunzi wa mwaka wa kwanza wananyimwa malazi baada ya kufunguliwa chuo tarehe 08/01/2007 wakitakiwa kukamilisha ada kwanza.
Ninachoweza kusema mimi,kulikuwa na utaratibu mbovu wa taarifa kuhusu ushirikishwaji uchangiaji wa gharama za elimu ya juu kwa 40%.Wazazi wengi hawafahamu kuhusu hilo na watakaomia ni wanafunzi.Inabidi bodi isahau kuhusu uchangiaji wa elimu na itoe mkopo kwa 100%,mwaka ujao wa masomo iandae programu nzuri na kila atakayechukua fomu za kujiunga na chuo chochote ajue atachangia kwa asilimia fulani.
Simu
0713803083
mikopo elimu ya juu
Submitted by Mwananchi on Wed, 2006-12-20 09:34.Jina
Mwl.mzeru,Deogratias Paul morogoro
Maoni
Nasikitishwa na hatua ya serikali kusitisha mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu shahada ya uzamili.(masters).kitendo hiki kinatufanya watanzania tushindwe kuingia kwenye soko la ushindani la ajira na pia kupoteza wataalamu ambao wangesaidia kuiletea Nchi maendeleo na kuwajengea uwezo wa kitaaluma.
Simu
0786 709600
Adhabu mashuleni
Submitted by Mwananchi on Mon, 2006-12-18 19:15.Jina
Emanueli shayo
Maoni
Mimi ninaomba viboko viondolewe mashuleni
Simu
0784751996
Daladala
Submitted by Mwananchi on Mon, 2006-12-18 17:02.Jina
Risper
Maoni
Moja ya sababu inayopelekea wafanyakazi wa daladala kukiuka miiko sahihi ya muongozo wa usafiri wawapo barabarani ni tamaa ya fedha iliyojengeka kati yao na matrafiki. Hivyo wapo tayari kufanya kila lisilostahili kwa sababu wanajua hata wakikamatwa watahonga kitu ambacho si sahihi. Kwa kifupi ndio hivyo.
Simu
daladala
Submitted by Mwananchi on Mon, 2006-12-18 16:02.Jina
Juma Richard Okumu
Maoni
tunaomba idara inayohusika na masuala ya usafirishaji ihakikishe kwamba watoto wanapata haki kama binadamu wengine ndani ya daladala .pia wahakikishe daladala zinawafikisha abiria mwisho wa safari kwa sababu kumekuwa na mtindo mpya wa kuwashusha abiria kabla ya kufika waendako.hii inatokea baada ya abiria wengi kushukia njiani na wachache wanaobaki hushushwa kabla ya kufika mwisho wa safari.ili kupunguza gharama ya mafuta.

