Kuvunjwa kwa Haki za Walemavu - CHUO KIKUU CHA DSM
Submitted by Mwananchi on Thu, 2006-11-02 10:18.
Jina
Shake
Maoni
<p>HAKIELIMU HONGERENI SANA KWA KAZI NZURI.</p><p>Pale Chuo Kikuu cha DSM, kuna bweni moja liliteuliwa kuwa ni bweni la walemavu na wasiojiweza (Disabled), bweni hili ni HALL SEVEN. Lakini cha kushangaza, miundombinu ya bweni hili haiendani na haiwawezeshi walemavu hao kuishi vizuri na kutumia mazingira ya bweni hilo kwa uhuru. Kwa mfano ukienda kwenye bweni hili utakuta VYOO na MABAFU ambavyo mlemavu asiye na miguu au ambaye anatembea kwa kushika chini (Kutambaa) hawezi kuvitumia na akabaki salama KIAFYA. </p><p>MBAYA ZAIDI, bweni hili halina MAJI yanayotoka bafuni wala vyooni. HII NI AIBU kabisa kwa chuo kikubwa kama hiki ambacho kinajulikana hadi nje ya mipaka ya Afrika, MAJI HAMNA VYOONI.....!? Hebu pata picha ya walemavu wale wanaotambaa huwa wanabebaje maji kwenda kwenye vyoo hivi vichafu? WATU WAKISHAJISAIDIA HAJA KUBWA, HAMNA MAJI YA KUFLASH. Upande wa dada na mama zetu hali ni mbaya zaidi hasa wanapokuwa katika vipindi fulani vya mwezi. </p><p>Kwa kweli hali hii inatisha na inatia aibu. Tunawaomba haki elimu kulirusha jambo hili hewani na waandishi wa habari ikiwezekana watembelee maeneo haya bila kutoa taarifa ili wakajionee wenyewe.</p>
