Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

Wapiga debe wa kituo cha mabasi Ubungo

Jina

Martin Jonas Kimbavala

Maoni

Wapiga debe kituo cha mabasi Ubungo ni kero kubwa sana kwa watumiaji wa kituo kile kikuu ikizingatiwa kile ni kituo kikubwa kinacho safirisha watu kuingia na kutoka nchi nzima na nchi jirani. Tabia inayokera zaidi ni kwamba wengi wao ni wezi wakubwa wanawaibia abiria fedha na mizigo yao. Napendekeza mkuu wa mkoa bwana Abasi Kandoro kama ameweza kuwaondoa wamachinga ahamie kwa hawa jamaa ikiwezekana wawekwe wanajeshi wa jeshi la kujenga taifa katika kituo kile kona zote za kituo kuhakikisha wanawatokomeza kabisa. Nimeshauri wanajeshi kwa sababu askari wa kawaida wanatabia ya kuchukua rushwa kutoka kwa wapiga debe hao jambo ambalo halitaweza kufanikisha suala zima la kuwaondoa.Wito pia kwa abiria wanaotumia kituo hicho wasiwape nafasi wapiga debe kuwachukulia mizigo na kuwapeleka kwenye mabasi wanayofanyia kazi washirikiane kikamilifu na askari watakao kuwa wamewekwa kituoni hapo.

Simu

Barua pepe

martjons@gmail.com
Vote Result
----------